Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Ihab Hamadeh, Mbunge wa Lebanon na mwanachama wa Kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama”, katika hafla kubwa iliyofanyika katika Husseiniyya ya kijiji cha Sharbin, eneo la Al-Hermel, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya tatu ya shahada ya shahidi Ali Khidr Nasir al-Din, iliyohudhuriwa na wanazuoni, familia za mashahidi, pamoja na idadi ya viongozi na wananchi, alisisitiza kwamba; silaha ya Muqawama, ambayo imekuwa kiwakilishi cha uwepo wetu, imethibitisha ufanisi wake katika kukabiliana na adui Muisraeli ambaye anaelewa lugha ya nguvu pekee, aliongeza kuwa; wale wanaoizungumza vibaya silaha hiyo wamejitenga na uhalisia na ukweli wa mambo.
Aliongeza kusema: “Adui Muisraeli anakabiliwa na matatizo na changamoto nyingi anapokutana na wapiganaji wa Muqawama, ambao wanaandika historis ya kishujaa iyo na mfano.”
Hamadeh anaamini kwamba; kuna kiwango kinachokubalika cha ushindi unaotarajiwa katika siku zijazo, na kwa kuwa ushindi huo ni wa kipekee, inahitajika kujitolea kipekee na damu za kipekee zinazohusishwa na Imam Hussein (as), ambaye katika siku hizi tunafanya majlisi za maombolezo ya shahada yake.
Maoni yako